Wednesday, July 6, 2016

KIOO lyrics by Janguar

One two, maisha ni kama safari ni safari
Hakuna ajuaye kesho itakuwaje

 
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo 
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo 

Maisha ni kama safari na yangu ishang'oa nanga
Tuna siku mbili muhimu, ya kuzaliwa na ya kuzama
Yangu ya kuzaliwa nishaijua bado ya kuzama toka duniani
Wanaongea sana na hawajui kule nimetoka
Wakisema na didimia, ona bado napepea 
Wakiniombea mabaya, duniani nazidi rusha zaidi yao
Wakidhani na didimia, ona bado napepea
Wakiniombea mabaya duniani nazidi rusha zaidi yao

 
  (CHORUS)
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo
Najiangalia kwa kioo, nijue tofauti ya jana na leo
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo
Najiangalia kwa kioo, nijue tofauti ya jana na leo

Nimetembea pote duniani nimepatana na wengi duniani
Kuna wale wananieleza ukweli wengine wananidanganya
Wengine hawalali wakitaka kushindana nami
Hawajui kule nimetoka hawajui yale nimeona

Wakisema na didimia, ona bado napepea 
Wakiniombea mabaya, duniani nazidi rusha zaidi yao
Wakidhani na didimia, ona bado napepea
Wakiniombea mabaya duniani, nazidi rusha zaidi yao

 
  (CHORUS)
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo
Najiangalia kwa kioo, nijue tofauti ya jana na leo
Najiangalia kwa kioo, kioo, kioo
Najiangalia kwa kioo, nijue tofauti ya jana na leo

 

No comments:

Post a Comment