Tuesday, July 26, 2016

UKIPENDWA RINGA lyrics by Z-Anto

[Intro]
Mmmh!
Mmmh!
Z-Anto, I’m back again

[Chorus]
Mtoto wa kike ukipendwa ringa (jishembendue)
Oh tena ringa (jishembendue) pozi jiachie
Kuna watu wanataka chance hiyo
Mtoto wa kiume ukipendwa vimba (tena jidekeze) tena vimba (tena jidekeze)
Jiachie, kuna watu wanataka chance hiyo
Ukinipenda, ntaringa
Nikikupenda, we ringa ila aah
Usije niumiza mi ntalia
Nikikupenda, we ringa
Ukinipenda, ntaringa ila aah
Usije niumiza mi ntalia

[Verse 1]
Mpenzi wangu wa kwanza nahifadhi lake jina
(Binti kiziwi) toka kwa moyo kidhati nilimpendaga
Nikaonyesha nampenda aka-change akasema ‘hanipendi tena
Enzi zangu zimepita’ hapo ndo akanimwaga

[Pre-Chorus]
Nilipoimba ‘nimebaki lonely, baki lonely’
Hata kitanda hakuna wa kunitandikia
Haki ya Mungu kuwa lonely, kuwa lonely
Hiyo ni adhabu kwa mtu aliyetimia
Nilipoimba ‘nipo lonely, nipo lonely’
Hata maji ya kunywa hakuna wa kunipatia
Haki ya Mungu kuwa lonely, kuwa lonely
Hiyo ni adhabu kwa mtu aliyetimia

[Chorus]
Mtoto wa kike ukipendwa ringa (jishembendue)
Oh tena ringa (jishembendue) pozi jiachie
Kuna watu wanataka chance hiyo
Mtoto wa kiume ukipendwa vimba (tena jidekeze) tena vimba (tena jidekeze)
Pozi jiachie, kuna watu wanataka chance hiyo
Ukinipenda, ntaringa
Nikikupenda, we ringa ila aah
Usije niumiza mi ntalia
Nikikupenda, we ringa
Ukinipenda, ntaringa ila aah
Usije niumiza mi ntalia

[Verse 2]
Kuhusu mapenzi yanaumizaga
Unapopenda we hupendwi sana hapo nashangaaga
Mapenzi yana siri gani aah
Tena naumiaga napokumbuka penzi langu kwake na ma-kiss kiss mwaah
Eti akanimwaga!

[Pre-Chorus]
Nilipoimba ‘nimebaki lonely, baki lonely’
Hata kitanda hakuna wa kunitandikia
Haki ya Mungu kuwa lonely, kuwa lonely
Hiyo ni adhabu kwa mtu aliyetimia
Nilipoimba ‘nipo lonely, nipo lonely’
Hata maji ya kunywa hakuna wa kunipatia
Haki ya Mungu kuwa lonely, kuwa lonely
Hiyo ni adhabu kwa mtu aliyetimia

[Chorus]
Mtoto wa kike ukipendwa ringa (jishembendue)
Oh tena ringa (jishembendue) pozi jiachie
Kuna watu wanataka chance hiyo
Mtoto wa kiume ukipendwa vimba (tena jidekeze) tena vimba (tena jidekeze)
Pozi jiachie, kuna watu wanataka chance hiyo
Ukinipenda, ntaringa
Nikikupenda, we ringa ila aah
Usije niumiza mi ntalia
Nikikupenda, we ringa
Ukinipenda, ntaringa ila aah
Usije niumiza mi ntalia

[Outro]
Unaemwacha leo ndio mpenzi mpya wa mwenzio
Hivyo kaba mpaka penati isijeeka kwako kilio
Unaemwacha leo ndio mpenzi mpya wa mwenzio
Hivyo kaba mpaka penati isijeikawa kesho kilio

No comments:

Post a Comment