Tuesday, July 26, 2016

NYOTA lyrics by Peter Msechu ft Amini

[Verse 1 – Amini]
Sikiliza rafiki, navumilia vingi vitimbwi
Moyoni bado anaishi, ila amejaa usaliti
Aliondoka akaniacha peke yangu
Huku nyuma nikalia na Mungu wangu
Haikufika hata mwezi, alipokosa furaha akarudi
Ameshachora na tattoo, jina la mpenzi wake mdanganyi
Lakini bado nilimpa moyo wangu
Nikiamini kuwa ye ni fungu langu, nilopangiwa

[Chorus – Peter Msechu] x2
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Kesha usiku na mchana ukiomba
Uzidi kusema na Mola ataitika

[Bridge – Amini]
Mapenzi ni wawili, wasioachana solemba
Iwe kwa dhiki, wingi wa mali
Muhimu kupendana
Mapenzi ni wawili, wasioachana solemba
Iwe kwa dhiki, wingi wa mali
Muhimu kupendana

[Verse 2 – Peter Msechu]
Mbona yako ni madogo
Yanayonikuta huwezi niamini
Mpaka leo naishi nae
Anakuja na mpenzi hadharani
Ninachofanya mi nacheza part yangu
Ingawa kidoleni ana pete yangu
Nakusihi vumilia, siku moja ndoto yako itatimia
Malumbano na zogo, ya mapenzi huwezi kimbia
Daima subira ndio ngao yangu
Nawe jaribu kufata nyendo zangu
Utajivunia

[Chorus – Amini] x2
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Kesha usiku na mchana ukiomba
Uzidi kusema na Mola ataitika

[Bridge – Peter Msechu]
Mapenzi ni wawili, wasioachana solemba
Iwe kwa dhiki, wingi wa mali
Muhimu kupendana
Mapenzi ni wawili, wasioachana solemba
Iwe kwa dhiki, wingi wa mali
Muhimu kupendana

[Chorus – Amini & Peter Msechu] x2
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Nyota na ing’ae kwako wee (nakuombea)
Kesha usiku na mchana ukiomba
Uzidi kusema na Mola ataitika

1 comment: