Thursday, July 21, 2016

KIPI SIJASKIA lyrics by Professor Jay ft Diamond Platnumz

[Verse 1] Professor Jay

Niliacha kazi nifanye mziki wakatabiri nitalosi

 Wengine wakanishawishi turoge kuondoa mikosi

Nakomaa na muziki ingawa jua la utosi

Naamini wote tunapita na kamwe maiti haijioshi

Jina langu lishatumika sana kutajirisha watu

 Nyota Ndogo alishasema kuna watu na viatu

Bunduki haiuwi watu ila watu ndio wanauwa watu

 Dunia kama jalala tazama kwa jicho la tatu

Ni saa mbaya watu wanahusda na roho mbaya

 Tunawaita watakatifu kumbe ndio ma vampire

Yalisemwa mengi demu wangu alivyotoroka

 Ni fundisho tosha na changamoto kwa mwanachoka

Nimepita mengi mitihani ya kila namna

 Ndio maana mi sishangai wakiniita mbeba lawama

Washkaji wengine fake kwenye deal hawakujui 

Wanadhani kila jogoo akiwika ni asubuhi

Riziki hamuezi iziba labda mtaichelewesha tu 

Mnakesha mnishushe mwenyezi ananipaisha

Kote mlikobana kidume ndo natusua 

Mnanijua nakamua roho za wanga zinaungua


[Chorus] Diamond

Unayehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde

Kwenye hii vita milele  nami nishike mkono nishinde

Unayehukumu ni wewe mwenyezi Mungu naomba unilinde

Kwenye hii  vita milele mwanachoka daima nishinde


[Verse 2] Professor Jay 

Walishazusha nimekufa eti nimepata ajali 

Washindwe na walegee Mwenyezi niepushie mbali

Wakasema nina ukimwi kwa kuwa nilikonda ghafla 

Wanataka kunizika mzima kabla sijafa

Waliosema nina ngoma wengine tushafukia 

Wanaomba nife leo naamini watatangulia

Mama pumzika pema daima tunakulilia

 Na bado  wanachonga sana but man the king is here

Daima mtaji wangu  ni nguvu zangu mwenyewe 

Simwamini mtu kamwe najiamini mi  mwenyewe

Hata nikinywa maji wanadhai nakunywa pombe 

Mi sijali I knock them hard mwanalizombe

Bado tunapambana kibarua kisiote nyasi 

Daima sitawadhuru wale wote walioniasi

Nikikaa kimya msidhani sijasikia

 Sio bahati sio ngekewa ni sauti iliobarikiwa holla

[Chorus] Diamond

Unayehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde

Kwenye hii vita milele  nami nishike mkono nishinde

Unayehukumu ni wewe mwenyezi Mungu naomba unilinde

Kwenye hii  vita milele mwanachoka daima nishinde

[Verse 3] Professor Jay

Mungu walaze pema waliyosemwa wakajiua

 Ingawa wote tunapita naamini maisha ni hatua

Maneno ya watu sumu yanaponya na yanauwa

 Please nipe  ujasiri mpaka siku  ukinichukua

Wape  nguvu wale wote waliokata tamaa

 Maneno yanaleta hila na mzozo kwenye mitaa

Wanahesabu mabaya tu na mema hawayaoni 

Wanakuchekea machoni wanakuroga moyoni

Wanacheka chinichini wakati una msiba

 Wa kwanza kukutangaza kwa watu ukiwa na shida

Wanatamani wapanguwe kila Mola alichopanga

 Wanatangaza amani huku wameficha mapanga

[Chorus] Diamond

Unayehukumu ni wewe Mwenyezi Mungu naomba unilinde

Kwenye hii vita milele  nami nishike mkono nishinde

Unayehukumu ni wewe mwenyezi Mungu naomba unilinde

Kwenye hii  vita milele mwanachoka daima nishinde 

Ta mi maneno nisha zoweya Ndo maana sijali wanapo ongeya

Wasema sema mengi mengi mengi


Ooh mi nimeshazoea  ndio maana sijali wanapo ongea  

Hey wanasema sema mengi mengi mengi ieee

Ooh ieee, tutuluuuluuu

5 comments: