Thursday, July 21, 2016

HISTORIA lyrics by Lady Jaydee

Unakubalije uwe historia
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia
Kabla siku yako haijafika

[Verse 1]
Muda huo, muda ulikuwepo
Muda huo uliopewa
Hela nazo zilikuwepo
Hela ulizobarikiwa
Maisha mazuri, nyumba nzuri
Gari nzuri na nini na nini
Muda huo uliuchezea
Pesa hizo ulizichezea
Kabla hata ya uzee haujaja
Wameshasea aah alikuwaga

[Chorus]
Unakubalije uwe historia
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia
Kabla siku yako haijafika

[Verse 2]
Tena hata, hata wenzio
Ulokuwa nao jana
Hata nao wanakusema
Mali na kukucheka
Umegeuka story
Umekuwa mfano
Geuka tukio, sio kivutio
Muda huo uliuchezea
Pesa nazo ulizichezea
Kabla hata ya kifo chako
Walishasema aah alikuwaga

[Chorus]
Unakubalije uwe historia
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia
Kabla siku yako haijafika

[Bridge]
Staki leo kuwa historia
Labda kesho iwe historia
Nataka niache historia
Ntakapofika kuwa historia

[Chorus]
Unakubalije uwe historia
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia
Kabla siku yako haijafika

Unakubalije uwe historia
Kabla siku yako haijafika
Iweje leo uwe historia
Kabla siku yako haijafika

No comments:

Post a Comment