Monday, June 27, 2016

YESU NDIYE SPONSOR lyrics by Jimmy Gait

OH nana na na OOH jimmy gait again
oh na na na na

kuna watu wako university na wengine wako jobless
wanashinda wakitafuta-tafutaa sponsor.
hawataki kufanya kazi  wanataka life so easy
wanashinda wakitafuta sponsor
utawapata Sarova wakiiwa wananyota
waone kama wanawezapata sponsor

 yesu ndie sponsor wa kweli ,
unapewa nyumba,  unapewa gari
na mali nyingi sana sana
mwishowe unajuta sababu yake sponsor
ndie sponsor wako anakufanyia wadhani niwe pekee,kumbe kuna kadha wa kadha
pia uwa anasponsor.
Wapata magonjwa yasiyo na tiba na future yako yatumbukia

njoo kwa Yesu sponsor wa kweli na hutajuta no no

chorus.x2

njoo kwa yesu sponsor wa kweli kila kitu atakupa oh oh
njoo kwa Yesu sponsor wa kweli na hutajuta no no

CHORUS.

Saturday, June 25, 2016

CHACUN POUR SOI lyrics by Papa Wemba ft Diamond Platinumz (Kila Mtu Kwake)

Motema ezo lela est ce que ozo yoka nga
Mawa na nga pe pinzoli eh
(Moyo unaniuma, hivi unaskia maumivu na machozi yangu?)
Mboka nini na kende epayi ya nga, Nakeyi Dar-Es-Salaam
(Niende wapi mbali na haya, nakwenda Dar-Es-Salaam)
Kolela na nga eleki ya moto mohumbu oya azangaki liberté
(Kilio changu kinazidi cha mutumwa asie kuwa huru)
Kuna kuna na Zanzibar
(Kule kule Zanzibar)

DIAMOND (PRE-CHORUS)
Alfajiri huwa ni kitendawili
Nafikiri pindi tukiwa wawili
Tena nakiri inanitesa mwili
Bora tu niache

   (CHORUS)
Chacun pour soi eh, mélodie na nga
(Kila mtu kivyake, melody yangu)
Chacun chez soi eh
(Kila mtu kwake)
Chacun pour soi eh, mélodie na nga
(Kila mtu kivyake, melody yangu)
Chacun pour soi eh
(Kila mtu kivyake)

Ukweli roho inanisonona
Tena moto hadi sijapona
Ila naamini Mola ataniona
Nitakuja pata wakuniponya
Ila tu chonde ma nikuombe
Usiniseme vibaya
Tena nakuombea kuongezewa
Kwa Mola mwaya

   (PRE-CHORUS)
Alfajiri huwa ni kitendawili
Nafikiri pindi tukiwa wawili
Tena nakiri inanitesa mwili
Bora tu niache
Nibaki mwenyewee

   (CHORUS)
Chacun pour soi eh, mélodie na nga
(Kila mtu kivyake, melody yangu)
Chacun chez soi eh
(Kila mtu kwake)
Chacun pour soi eh, mélodie na nga
(Kila mtu kivyake, melody yangu)
Chacun pour soi eh
(Kila mtu kivyake)

Aah chacun soi eh
(Kila mtu kivyake)

   (CHORUS)

Tucheze rumba
Tena taratibu na mtumba
Twapenda rumba
Wote na marafiki wa kunyumba
Cheza rumba
KINSHASA
Tobina rumba
NAIROBI
Cheza rumba
BRAZZAVILLE
Tobina rumba
Cheza rumba
ABIDJAN NA YAOUNDE
Tobina rumba
NA COTONOU LOME
Mambi na mwana Africa
Rumba ya bana mboka
(Rumba ya wananchi)

Tuesday, June 14, 2016

SUU lyrics by Yamoto band ft Ruby

Wee Ruby karibu mkubwa na wanawe
Haya haya ×4

Nachojua undugu ni ule wa damu, kuzaliwa tumbo moja
We na mimi hatunaga uharani, basi punguza uonga
Nitakupa mapenzi matamtam
Napendaga namba moja
Pilipili yawasha lakini tamu tunapozanga na soda
Nitamushawishi mama, amupende sana babaako
Tutakuchezea chezea, mdogo mdogo utazowea

Kupiga selfie selfie kila siku hazina maana
Nitadondosha simu makusudi, tuonekane hatuna maana ×2
Turuba initandikie, naamusha usimamie
We mtoto wa baba Eh! Eh! Eh!

Undugu kaunganusha baba, kwa mama yenu nyie
Mnapaswa muniite dada na muniheshimu mie ×2
Kweli baba anaishi kwa mama yenu
Naomba sana dada yenu munieshimu

  (CHORUS)
Hili zizi la kondoo dume
We ni apple lazima uchumwe
Acha niombe mungu kidume aye-ye-ye-ye

Suu nitamwambia baba
Nitamwambia baba
Nitamwambia baba
Munanisumbua ×2

Ruby, mama kaniambia nioe-nioe-nioe
Ila mimi nataka nikuoe wewe Ruby
Ayii Ruby!
Basi punguzanga kiwewe
Niruhusu Ruby na mimi nikuite baby
Hapana aaa
Funika kombe mwana haramu apite, apite
Mimi kwako wewe nitakifanya chochote, chochote
Ruby si dada yangu kusema tumetoka wote kwa mama yangu
Ukinipenda akitokei chochote
Pam Pam ru-ma
Mlango wa chuma, ukiufungua hauna
huruma
Mama anataka mjukuu, yani ni kuweka usiku
Pam Pam ru-ma
Mlango wa chuma, ukiufungua hauna huruma
Wouho, wouho, iyoo mama
Yo iyo, yo iyo
Iyoo mama, mame eeh!

Kwanza moja nikwambie, wewe unaendana na mie
Wengine we wakunjie, ni mimi tu niwe na wewe
Nataka kufurahisha baby, komando nitalinda kidonda
Nzi wasije fonza nitaumia
Usiku waaga vinanitoka, mi siri ya bomba nimefunguka
Nahisi waniita mwenzako pwa ka cha lishafunguka 

  (CHORUS)

Monday, June 13, 2016

MOYO MASHINE lyrics by Ben Pol

Najua kukikucha ntajuta kama nikikuta unanitania
Maana moyo wangu nimekupa uweke
Mimi ni mfungwa tena mjinga
Nimejileta gerezani
Tena sikuwaza nitakuwa mateka mmmh

  (PRE-CHORUS)
Najua ulinizungusha sana
Sijali huwa ni mambo ya ujana
Kukupenda wewe sijuti
Maneno yalisemwa mengi sana
Kuna wakati nilikata tamaa
Kukupenda wewe sichoki

  (CHORUS)
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha wasema)
Nimekupendea nini
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo uloshakosaga
(Wacha waseme)
Nimekupendea nini

Nafsi inanituma upendo uko nje ya maneno, ila vitendo
Kama bubu akipenda atanena vipi kwa maneno
Pasina vitendo?
Kiziwi, ata ukimwambia nakupenda wala hasikii
Ila vitendo ooh
Wewe sijui sababu za kukupenda
Siwezi sema, ila utaona aah

  (PRE-CHORUS)
 
  (CHORUS)

Ooh kama moyo ulisimama nilipokuona
Hukuongea, hukucheka, nilikuona tu
Na tabia sikufahamu, labda niache mwanadamu
Ukipenda usishangae ni upofu wa moyo
Kumbe moyo ulinirubuni, hukusema umependa nini

  (CHORUS)

Saturday, June 4, 2016

IBAKI STORY lyrics by Rich Mavoko

Matapishi ni kinyaa, kuzirudisha tena kwenye kinywa
Japo mengi ulisema, kama nuru ghafla ukazima
Ikawa ngumu kukusahau, nikasema moyo ukome
Kwa kali sulu na madharau, penzi ulivunja na ngome 

   (PRE-CHORUS)
Na unajua ata nikilia siwezi kutokwa na machozi
We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo
Aah ukaudhulumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo
Leo unatamani wewe kurudia zamani ni ndoto
Wewe ni rubuni kwa penzi la kidani kama mtoto

  (CHORUS)
Mi na wewe, acha ibaki story mina wewe
Mapenzi mina wewe, acha ibaki story mi na wewe
Mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe

Kiliniumiza kitanda na shuka tuliolalia
Mapenzi yana siri kubwa, sishangai mtu akilia
Nimekubali mboni zangu, zimtazame mwingine
Maridhia ya moyo wangu, huenda si fungu pengine
Cha kushangaza hadharani mengi ya kuficha ukaweka wazi
Nikahisi sijui mapenzi labda kwako sinogi nazi 

  (PRE-CHORUS)
Na unajua hata nikilia siwezi kutokwa na machozi
We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo
Aah ukaudhurumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo
Leo unatamani wewe kurudia zamani ni ndoto
Wewe ni rubuni kwa penzi la kidani kama mtoto

  (CHORUS)

Yalinitesa mazoea aya lakini nishazoea mwaya
Ila tambua mapenzi mabaya, kidonda chake hakinanga dawa
Eeh mazoea aah, lakini mi nishazoea mwaya
Ila tambua mapenzi mabaya, kidonda chake hakinanga dawa

  (CHORUS)