Tuesday, July 26, 2016

TATHMINI lyrics by Professor Kay and other Artists

[Verse 1 – Professor Jay]
Naahidi kuwa makini mpaka siku nafukiwa chini
Na Mungu aliye hai bado yu pamoja na mimi
Emcee shika vizuri karibu tawi linakatika
Na kwa wote mliopo juu na chini sauti itafika
Kazi na dawa ndani ya uswazi kazi ni kazi
Na nipo radhi kutoa tathmini ngazi kwa ngazi
Rap si lelemama kama wengi mnavyodhani
Fasihi iliyo hai kuitoa jamii gizani
Miaka ya 80 Hip Hop Bongo ilichipua
Na nadhani wale wakongwe wa rap hii mnaitambua
Hali ilikuwa mbaya miaka ya 89
Watu hawakutaka kuelewa rap kabisa
Miaka ya 90 Hip Hop Bongo imekubalika
Wenye nia nzuri na rap tunawajibika
Rap ni wito yataka utashi na ufahamu
Elimu ya mtaani kujituma pia nidhamu
Wasanii wenyewe wa Bongo tunaofanya tudharauliwe
Watu vibongo vidogo hawataki washauriwe
Wanaongea blah blah, vijino viwe
Na wanaovunja hata miko ya rap waheshimiwe!
Wengine watatumia kivuli cha rap kufanyia uhuni
Hii ni sawa na kupanda ngazi kuelekea mbinguni
tathmini ya kweli yatia majaribuni
Na mnaovunja miko ya rap jihukumuni

[Hook – Professor Jay] x2
Hii ni tathmini kwa wote juu na chini
Yoh emcee zunguka nyuzi 360
Umeona nini? Mwana mpotevu rudi kundini
Fani ni uwanja mpana na jua lipo utosini

[Verse 2 – Jay Moe]
Yoh! Mawazo ya Jay Moe usiku mchana yalikuwa wima
Ingawa sikujua usiku ukiisha asubuhi itakuwa neema
Kwani baba mama miaka ile kipindi cha nyuma
Waliamini rap ni kuimba yale yasiokuwa mema
Haina noma wakwezi tulipomaliza kusoma
Mistari iliandikwa ujumbe ukashuka ukakubalika
Ndio ilikuwa bado wenye hisa kutolea macho
Walithamini Bolingo, ambacho kimewachosha Bongo
Wahisani waongo, walidhani tungedorola
Mara ngoma ika-change na nyota ya rap ikang’ara
Wasambazaji habari ya kwamba Hip Hop uhuni
Wameingia mitini ‘Chemsha Bongo’ ilipoingia redioni
Kama wametawala ikafika walio bungeni
Watu wakazinduka, yaani wakashtuka wataongea nini
Watu na Bongo Flava kingine wanasema uzushi
Taarabu imeingia nuksi, Bolingo inafuka moshi
Sasa wahisani tapeli hutuboa wenye mistari
Kila mtu anakuja na uongo ili mradi tukubali
Na ma-producer wa sasa wanashtuka kwamba tunauza
Wanashtuka kwamba walicheza, Hip Hop ina fedha
Jay Moe mbakiaji sasa nahitaji umaskini u-bounce
Shori mzuri, gari, pamba, fedha kwenye bank account
Labda tatizo iwe kwa emcee asiye na elimu
Eti afanye nini? Mi nadhani bora akauze ndumu

[Hook – Professor Jay] x2
Hii ni tathmini kwa wote juu na chini
Yoh emcee zunguka nyuzi 360
Umeona nini? Mwana mpotevu rudi kundini
Fani ni uwanja mpana na jua lipo utosini

[Verse 3 – Professor Jay]
Yule yule ni Jay na Jay ni yule yule
Wanga wekeni kikao kisha mnifanye msukule
Domo langu ni hela linatoa ushauri wa bure
Ila ma-emcee wengi wa Bongo hampendi kwenda shule
Kumbuka hii ni rap ndani ya karne ya 21
Ni lazma uchemshe bongo kwenye mchanganuo wa hoja
Nafurahi kuona emcees ni wengi kama utitiri
Kinachoniudhi wengi wana-rap bila kutumia akili
Rap ya Bongo imegawanyika makundi mawili
Na kuna ma-emcee kamili na emcee waliobatili
Emcee mwenye hekima anafikiri kabla ya ku-rap
Na emcee mpumbavu ana-rap apate nyapu
Natumia lugha kali tafsiri unavyoweza
Napunguza tafsida maneno yanajieleza
Watu viwango vidogo wanaleweshwa na sifa
Ni lazma mjikongoje kwenye level za kimataifa
Wengi hampendi kuchambua temethali za semi
Na matokeo ndo vile ngoma zenu mwali hanemi
Watu wanavaba mic na ku-rap kama majuha tu
Katikati ya bahari mnapanda boti za mabua
Msilete utani, hii ni fani yenye ushindani
Jiulize waliovuma wangapi wamebaki gizani
Ninaowaudhi, hii naifanya makusudi
Ili mpate ghadhabu na kuongeza juhudi

[Hook – Professor Jay] x2
Hii ni tathmini kwa wote juu na chini
Yoh emcee zunguka nyuzi 360
Umeona nini? Mwana mpotevu rudi kundini
Fani ni uwanja mpana na jua lipo utosini

No comments:

Post a Comment