Tuesday, July 26, 2016

MAMA lyrics by Peter Msechu ft Banana Zorro

[Verse 1 – Banana Zorro]
Niulinganishe na nani, ukarimu wa moyo wako?
Nikulinganishe na nani, sijaona mfano wako
Vita ya vituko vyangu, mambo yote mabaya yangu
Bado uko karibu yangu wewe
Kuna wakati sirudi nyumbani na starehe za mjini
Awakumbatia watoto, waonyeshe picha zangu mimi
Wewe wa kipekee, mpenzi wangu
Wewe ndio mama yangu, oh oh
Sina hata pa kugeukia, pa kukimbilia
Unanivumilia sana, oh mama
Mmh, oh mama, mama Sangira
Oh mama wanangu mama, ey
Sijui hata wanangu shuleni wanavaa vitu gani
Sijui hata wanangu kule wanakulaga nini!

[Chorus – Peter Msechu & (Banana)]x2
Oh mama, oh mama, oh mama
(Mama Sangira mama)
Oh mama, oh mama, oh mama
(Mama Sangira mama)

[Verse 2 – Peter Msechu]
Binadamu binadamu, baba Ayamu na mwingine
Si unakumbuka alisema nimerogwa sehemu nyingine?
Sijapinda mamaa, sijageuka
Sijui kipi kinaniharibu, wowowoo
Moyo wako sijaona wa kufananisha nae
Nilikupata kwa bahati tu mamaa
Wazazi walipinga mimi kuwa nawe
Wazazi walipinga mimi kuoana nawe
Ona nilikataa sikusikiiza, sikusikiiza mie
Ndo maana niko nawe, nipende mamaa
Nipende mama Lolo na ubaya wangu mamaa

[Chorus – Peter Msechu]
Oh mama, oh mama, oh mama
(Na ubaya wangu mama)
Oh mama, oh mama, oh mama
Oh mama, oh mama, oh mama
Oh mama, oh mama, oh mama

No comments:

Post a Comment