Wednesday, July 6, 2016

KIGEUGEU lyrics by Janguar


Dunia nizamishe ama uniweke niishi pekee yangu
Kwani ninapomwamini kila binadamu, mwishowe ananigeukia ×2

  (CHORUS)
Nimtazame nani, nimwamini nani (nani)
wananigeukia
Vigeugeu... vigeugeu... vigeugeu wananigeukia ×2

Namwamini daktari sana amponye
rafiki yangu
Anamweka kwenye life support machine,
kumbe aliaga ni pesa anakusanya
Mama mzito anamwamini mkunga
amzalishie mtoto baada ya miezi tisa, mkunga anamgeukia
Mtoto anamgeuzia

Niki-hustle juu chini ili nivuke border
wananigeukia
Niki-hustle juu chini ili nivuke border
wananigeukia ×2

  (CHORUS)

Mwanasiasa aliniomba kura akiniahidi yote atatimiza
Baada ya miaka tano anarudi na kitambi
bila kutimiza
Nina pastor ka jirani yangu nilimwamini
kufa na kupona
Nikitoka kwangu, naye anaingia kuzali
na bibi yangu

Niki-hustle juu chini ili nivuke border
wananigeukia
Niki-hustle juu chini ili nivuke border
wananigeukia ×2

  (CHORUS)

Dunia nizamishe ama uniweke niishi pekee yangu
Kwani ninapomwamini kila binadamu, mwishowe ananigeukia ×2

Bibi yangu kigeugeu
Pastor wangu kigeugeu
Mkunga kigeugeu
Wanasiasa vigeugeu
Rafiki yangu kigeugeu
Fundi wangu kigeugeu
Dereva, kigeugeu
Conductor, kigeugeu ×2

No comments:

Post a Comment