Thursday, July 21, 2016

NATAMANI KUWA MALAIKA lyrics by Lady Jaydee

[Chorus] x2
Natamani kuwa malaika
Natamani tena kurudi nyuma
Natamani kuwa kama zamani
Natamani kuwa kama mtoto

[Verse 1]
Moyo wangu mweupe kama theluji
Si mawazo mabaya wala chuki duniani ooh
Tabasamu hata kwa adui
Kuishi bila kulipa bill
Nikilia nabembelezwa si sasa nabezwa
Nikichoka tembea nabebwa
Kila kitu mimi nafanyiwa
Malaika, mtoto ni malaika

[Chorus] x2
Natamani kuwa malaika
Natamani tena kurudi nyuma
Natamani kuwa kama zamani
Natamani kuwa kama mtoto

[Verse 2]
Kama mimi nisingekuwa mkubwa
Katu nisingejua adha za dunia
Majukumu nisingefikiria
Kulala muda ninao amua
Stress zisingenifika
Majaribu nisingepata
Machungu nisingehisia
Kama hii leo nisingekuwa
Natamani kuwa malaika oooh

[Chorus] x2
Natamani kuwa malaika
Natamani tena kurudi nyuma
Natamani kuwa kama zamani
Natamani kuwa kama mtoto

[Bridge]
Mnasema ukubwa raha
Lakini mzigo mkubwa
Ukubwa jalala
Kila unapozidi kua
Manyang’au yakutamania
Tamania kukuraruaa

[Chorus]
Natamani kuwa malaika
Natamani tena kurudi nyuma
Natamani kuwa kama zamani
Natamani kuwa kama mtoto

No comments:

Post a Comment