Monday, July 25, 2016

WANAUME KAMA MABINTI lyrics by Lady Jaydee ft Papii Kocha

[Chorus – Lady Jay Dee]
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti

[Verse 1 – Lady Jay Dee]
Hivi nini kimewauma? Sikumaanisha wote
Na kama kweli hakikuhusu, hakiwezi kuuma
Najua wazi mnaelewa, ila mu wabishi
Hamtaki kukubali huu ukweli halisi
Vyovyote itavyokuwa ujumbe wangu mmeupata
Hata mkijifanya hamtaki vyema kuelewa
Fanyeni kazi vijana ili tuijenge nchi
Kamwe msikubali kufananishwa na machangudoa

[Chorus – Lady Jay Dee]
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti

[Verse 2 – Papii Kocha]
Ebwana sema, sema, sema, haki yako Jay Dee
Tembo kuvaa vipusa halali haki yako Zey D
Inakuwa vipi wanaume muwe tegemezi?
Japokuwa kweli wamama wanawapeni mapenzi
Mkivishwa magauni na vimini mtachukia
Acheni basi kama hamtaki, ya kuambiwa ukweli ukweli

[Chorus – Lady Jay Dee]
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti

[Verse 3 – Lady Jay Dee]
Ukiwakuta kwenye vikao, oh vya pombe
Eti wao wasemaji, wanaojua yote
Hawatoi hata senti ya kulipa bili
Ikifika zamu yao huenda msalani
Kwa ukuwadi namba moja wao hupenda
Wanaopenda kuwaliwaza mademu wa wenzao
Shoga zangu hebu leteni magauni tuwavishe
Hijabu tuwafunge, na vimini, vitopu tuwaazime

[Chorus – Lady Jay Dee]
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti

[Bridge]
[Lady Jay Dee]
Papii umeona wapi mwanaume kunyweshwa pombe?

[Papii Kocha]
Jay Dee hivi tangu lini, rijali zima likasutwa?!

[Lady Jay Dee & Papii Kocha]
Nilishangaa ya jana, ati nae kaja kitchen party, olala

[Chorus – Lady Jay Dee] x2
Mnakula, kunywa na kuvaa siku zinaenda
Vya bure hupenda kupewa, wala hamna fikira
Kila upande mna-fit, siku zinaenda
Vinywa vimejaa ufitini, wanaume kama mabinti

[Outro – Papii Kocha & (Lady Jay Dee)]
Igwe, igwe lele lele (igwe lele lele)
Igwe, igwe lele lele, ah, ah, igwe lele lele
Igwe lele lele, ah, ah, igwe lele lele
Lele lele (lele lele) ah, ah, igwe lele lele
(Igwe lele lele)
Igwe, igwe lele lele (igwe lele lele)
Igwe yoyo, igwe lele lele
Igwe, igwe lele lele (igwe lele lele)
Ah, ah, ah, ah, igwe lele lele
Lady Jay Dee, uko Papii Kocha eeh
(Mika Mwamba, na Norman Dikaka)

No comments:

Post a Comment