Wednesday, July 13, 2016

WATU NA VIATU lyrics by Nyota Ndogo

Rafiki yangu, mpendwa
naja kwako, siku nyingi
wanipokea, kwa uzuri
siku zote
wakati sina, wanipa
nitakacho, husiti
nisemacho, wako sawa waniombea Mungu
moyoni mwangu, najua
nina rafiki, huyu wa kweli
hakuna yule, ambaye
atakuja, kati yetu
wakati sina, wanipa
nitakacho, husiti
nisemacho, wako sawa waniombea Mungu

  (CHORUS)
oh kuna watu na viatu duniani
oh kuna watu wasiopenda maendeleo
ukiwa nacho chawauma ndani kwa ndani
achana nao, waepuke haraka sana

hivi majuzi nilipata kazi nzuri nikaja kukueleza
mtu wa kwanza nilifikiria ni wewe rafiki yangu
nilifurahi na kuruka na kutaja jina lake Mungu
nikikuangalia mwako usoni umejisononesha
ukaanza kusonya, ukirusha mikono
sura umeikunja, kumbe hukufurahi
mafanikio yangu, ilikuwa hatia mimi kuja kukueleza
ukaanza kusonya, ukirusha mikono
sura umeikunja, kumbe hukufurahi
mafanikio yangu, ilikuwa hatia mimi kuja kukueleza
mtu wa kwanza nilifikiria ni wewe rafiki yangu

  (CHORUS)
oh kuna watu na viatu duniani
oh kuna watu wasiopenda maendeleo
ukiwa nacho chawauma ndani kwa ndani
achana nao, waepuke haraka sana

No comments:

Post a Comment