Thursday, July 21, 2016

PETE lyrics by Ben Pol

[Verse 1]
Hadithi ya penzi langu naikata ni ni mwisho oh
Huthamini, huoni pendo lako nalihitaji leo kesho oh
(Nshawahi kukosa) mwenzenu nilisumbuka mchana na usiku mimi
(Nshawahi kukosa) nasema niliteseka mchana na usiku mimi
(Nshawahi kukosa) mwenzenu nilisumbuka mchana na usiku mimi
(Sihitaji tena kosa) najua nitateseka mwisho sitakuwa nawe tena, nauliza…

[Chorus] x2
Ni kama pete yangu inakuchoma kidoleni
Ni kama pendo langu linakuchoma moyoni
Bora kuitoa a haa, pendo kulivua aaah
Bora kuitoa, moyoni mwangu mi nisiteseke
Bora kuitoa a haa, pendo kulivua aaah
Bora kuitoa, moyoni mwangu mi nisiteseke

[Verse 2]
Ah! Sikujali wambea wanafki walosema
Hatutodumu mimi nawe tutaja achana
Wakiniona siko nawe si ndo watasema
Hata nyumbani watajua tumefarakana

[Bridge 1]
Nikiwaza kwenda mbali, moyoni nahofia
Maana bado nakujali, kwako nilishatua
Nikiwaza kwenda mbali, moyoni nahofia
Maana bado nakujali, kwako nilishatua

[Bridge 2]
Na kila jema nitendalo (mie)
Kwako limekuwa sio (mie)
Nitakapo kujua ulipo (mie)
Wanijibu utakavyo
Pete kidoleni mwako, yanisuta mwenzio (mwenzio)
Ndo maana nikukosapo, moyo wanienda mbio
Uuhh ooo yeeeah!

[Chorus] x2
Ni kama pete yangu inakuchoma kidoleni
Ni kama pendo langu linakuchoma moyoni
Bora kuitoa a haa, pendo kulivua aaah
Bora kuitoa, moyoni mwangu mi nisiteseke
Bora kuitoa a haa, pendo kulivua aaah
Bora kuitoa, moyoni mwangu mi nisiteseke

[Outro]
Ohh mmhh
Classic Sound
Aaah new Ben Pol

No comments:

Post a Comment