Wednesday, July 13, 2016

NALIA lyrics by Nyota Ndogo


Pakuenda sina, wakunipokea hakuna
machozi yanitoka, tabasamu sina
kila niendapo watu wanitusi
eti sina kwetu, mie mtumishi
mtoto wa watu, nimekosa nini
hakuna anipendaye, basi niambieni

  (CHORUS)
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza

Baba akaniacha, mama akanitoroka
mjomba akanifukuza, shangazi hanitaki
mpaka lini mimi, nitaishi hivi
nitambulisheni, nami nielewe
kosa langu nini, mi mja wa Mungu
basi niambieni, nami nielewe

  (CHORUS)
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza

Nahitaji jibu, mbona mkokimya
nifafanulieni, nataka kujua
sasa nyie nyote, mmenikimbia
mie mwana wenu, niende kwa nani

  (CHORUS)
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza

Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza
Ooh nalia hakuna wa kunibembeleza

No comments:

Post a Comment