Najutia upendo, maana kutendwa ni maumivu
Moyoni n’na pengo, kitovu cha mapenzi kweli ni wivu

Verse 1
Ulimi ulikosa, kwa matamshi machafu machafu sana
Penzi limekufa, limeshaliwa na wafu inaniuma sana
Unaamini kwamba, ukipandacho ni sumu ndani ya moyo wako
Labda ungejifunga, usingejilaumu ndani ya penzi lako
Zile ndoto za mchana aaah
Kwa kudanganywa utapendwa aaah
Kwa marefu na mapana aaah
Ona yule mi nakwenda aaah
Zile ndoto za mchana
Kwa kudanganywa utapendwa
Kwa marefu na mapana
Ona yule mi nakwenda hey!
CHORUS
Najutia upendo, maana kutendwa ni maumivu
Moyoni n’na pengo, kitovu cha mapenzi kweli ni wivu
Najutia upendo, maana kutendwa ni maumivu
Moyoni n’na pengo, kitovu cha mapenzi kweli ni wivu
Verse 2
Uliukimbiza upepo, kwa kujua nini utapata
Umeambulia mateso, moyo umebaki unajaka
Kama Kinyonga tabia zangu, kila siku nabadilika
Hukuyaelewa matendo yangu, si kwa kiangazi wala masika
Ukavunja na ukimya aah
Ukasema hisia zako aah
Mwenzako mbona nipo kimya aah
Ooh! Nalia na penzi lako aah
CHORUS
Najutia upendo, maana kutendwa ni maumivu
Moyoni n’na pengo, kitovu cha mapenzi kweli ni wivu
Najutia upendo, maana kutendwa ni maumivu
Moyoni n’na pengo, kitovu cha mapenzi kweli ni wivu
No comments:
Post a Comment