Friday, July 15, 2016

MZIKI GANI lyrics by Nay Wa Mitego ft Diamond Platnumz

  CHORUS
Hivi nyi ma mc mnachoimba kitu gani, mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).

Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney)  X2 

DIAMOND
Hata bibi yangu mi aliniambia , mwanamke anahitaji kubembelezwa

Kupetipeti matunzo pia, ukienda rafu utampoteza,

Muziki ni mfano wa binti muzuri,

Na ndio maana namtunza kwa   vazi na uturi

NEY WA MITEGO
Aaah piga kimya, we ndo haufai kabisa hauna maana

Wabana pua kila siku mnarogana, bibi yako alikuambia muziki ni kama binti

Mbona unawachezea unawatema kama big g

Mara wema, mara Jo keti, mara Naj, mara Penny, je mnafanya mziki mpate mabinti

DIAMOND
Uuuhhuuuu, hata wazee wazamani, walishasemaga kazi na dawa

Chamuhimu jukwaani, ni kuhakikisha wanapagawa,

Kwa michezo ya kuringa ringa  ndo huwa wanadata

Badilika usiwe mjinga, utawakamata

  CHORUS

Hivi nyi ma mc mnachoimba kitu gani, mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).

Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney)  X2 

NEY WA MITEGO
Muziki wenu ushirikina ndio umetawala, q chilla analalama anasema umemroga

 Mganga wako aliekutoa umemkimbia hujalipa,  bila skendo za magazeti basi huskiki

DIAMOND
Mi ni mti wenye matunda, milele siogopi kupigwa mawe

Ubaya wenu wengi kayumba, elimu mliitupa sandakalawe

NEY WA MITEGO
Bado hujanishawishi, bongo fleva inanipa kichefu chefu

Kwanza nyie malimbukeni wa umaarufu

Mnalenta maringo mpaka kwa mashabiki , Wabana pua nyie watoto sio riziki,

Mnavaa nguo za dada zenu, zinawabana mapaja nyie makaka duu

Aah nyie watoto mchele mchele , kwenye show viuno mbele mbele X2

Nimewanyamazisha, brazameni vipi  we bado unabisha

DIAMOND
Mi nnamengi nnayajua, ila we ni mtemi utaanzisha utata

Michezo yenu kutoboa pua, bora ninyamaze usinipige mbata

CHORUS
Hivi nyi ma mc mnachoimba kitu gani, mara bangi mara matusi sa ndo muziki gani (diamond).

Hii no hip-hop h.o.p muasisi wa burudani, tushachoshwa kutwa mapenzi, kabane Pua nyumbani (ney)  X2

No comments:

Post a Comment