[Verse 1]
Nilikuwa na mpenzi wangu, nani asiyemjua
Mtoto kaumbika, utasema malaika
Miezi kadhaa ikasogea, mtoto wa kwanza tukazaa
Mtoto katoka mwarabu, swali lilikosa jibu
Akasema we hujui, mtoto kafata kwa babu
Nikaguna guna pale mzee, nikauchuna
Mtoto wa pili tukazaa, huyu wa sasa mchina, duh!
Nikasema mama vipi, mbona mi sielewi!
Akasema we hujui, huyu kafata kwa bibi
Mzee naibiwa, mzee naonewa
[Chorus] x2
Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?
(Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?)
Awe mama wewe, uwe ungefanyaje?
(Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?)
[Verse 2]
Mwenzenu nalala chini, mke wange kitandani
Nikilala kitandani, kila mtu shuka lake
Mwenzenu nalala chini, mke wange kitandani
Nikilala kitandani basi ujue mzungu-wa-nne
Nikiuliza kwanini, anasema amenipa likizo eh
Nikiuliza kwanini, anasema amenipa likizo eh
Sio kama napenda, imenilazimu
Sio kama napenda, ananilazimisha yo
Mwenzenu naosha vyombo, mwenzenu napiga deki
Mzee mzima napika, jamani nafua nguo
Sio kama napenda, nalazimishwa mimi
Sio kama napenda, nalazimishwa mimi
[Bridge]
Uliniacha na mtoto wangu mdogo Vanessa eh
Miaka inakwenda, siku zinarudi mimi na Vanessa eh
Wewe utakuja nikumbuka
Wewe utakuja niuliza
Gigigi mapenzi na wewe sasa yamekwisha
Usinijue jue, usinitambue
Oh chunga nyumba na mama Vanessa eh
Oho chunga nyumba na mama Vanessa eh
Fadena mapambano yo
[Chorus] x2
Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?
(Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?)
Awe mama wewe, uwe ungefanyaje?
(Awe mama wee, ingekuwa ungefanyaje?)
[Outro]
Mke wangu mwanajeshi, mwenzenu nafua gwanda
Nikileta ubishi, ananipiga mashuti
Jana kaniambia eti nimsindikize gesti
Ila nimsubiri kwa nje eti anaenda kuongea mambo ya business
Ameenda kugombana na mashoga zake
Halafu ananiambia eti mi niende nikasute
Leo kanifukuza chumbani eti nitoke nje
Kisa anavaa nisije nikamchungulia
An inspiring song
ReplyDeleteYears after.. Still love this song
ReplyDeleteVery nice song
ReplyDeleteKwetu Rwanda bado tunaupenda wimbo huu, wimbo wa milele!
ReplyDeleteThis song, grew up while it was hitting.. years later I still search for its lyrics.
ReplyDeleteU look so song
ReplyDelete