Monday, June 13, 2016

MOYO MASHINE lyrics by Ben Pol

Najua kukikucha ntajuta kama nikikuta unanitania
Maana moyo wangu nimekupa uweke
Mimi ni mfungwa tena mjinga
Nimejileta gerezani
Tena sikuwaza nitakuwa mateka mmmh

  (PRE-CHORUS)
Najua ulinizungusha sana
Sijali huwa ni mambo ya ujana
Kukupenda wewe sijuti
Maneno yalisemwa mengi sana
Kuna wakati nilikata tamaa
Kukupenda wewe sichoki

  (CHORUS)
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo ulishakosa
(Acha wasema)
Nimekupendea nini
(Moyo mashine)
Ila majibu ya upendo uloshakosaga
(Wacha waseme)
Nimekupendea nini

Nafsi inanituma upendo uko nje ya maneno, ila vitendo
Kama bubu akipenda atanena vipi kwa maneno
Pasina vitendo?
Kiziwi, ata ukimwambia nakupenda wala hasikii
Ila vitendo ooh
Wewe sijui sababu za kukupenda
Siwezi sema, ila utaona aah

  (PRE-CHORUS)
 
  (CHORUS)

Ooh kama moyo ulisimama nilipokuona
Hukuongea, hukucheka, nilikuona tu
Na tabia sikufahamu, labda niache mwanadamu
Ukipenda usishangae ni upofu wa moyo
Kumbe moyo ulinirubuni, hukusema umependa nini

  (CHORUS)

1 comment: