Saturday, June 4, 2016

IBAKI STORY lyrics by Rich Mavoko

Matapishi ni kinyaa, kuzirudisha tena kwenye kinywa
Japo mengi ulisema, kama nuru ghafla ukazima
Ikawa ngumu kukusahau, nikasema moyo ukome
Kwa kali sulu na madharau, penzi ulivunja na ngome 

   (PRE-CHORUS)
Na unajua ata nikilia siwezi kutokwa na machozi
We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo
Aah ukaudhulumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo
Leo unatamani wewe kurudia zamani ni ndoto
Wewe ni rubuni kwa penzi la kidani kama mtoto

  (CHORUS)
Mi na wewe, acha ibaki story mina wewe
Mapenzi mina wewe, acha ibaki story mi na wewe
Mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe Mapenzi mi na wewe, acha ibaki story mi na wewe

Kiliniumiza kitanda na shuka tuliolalia
Mapenzi yana siri kubwa, sishangai mtu akilia
Nimekubali mboni zangu, zimtazame mwingine
Maridhia ya moyo wangu, huenda si fungu pengine
Cha kushangaza hadharani mengi ya kuficha ukaweka wazi
Nikahisi sijui mapenzi labda kwako sinogi nazi 

  (PRE-CHORUS)
Na unajua hata nikilia siwezi kutokwa na machozi
We ndo ulifanya macho yangu nione wengi waongo
Aah ukaudhurumu moyo wangu, uliuza penzi kwa magendo
Leo unatamani wewe kurudia zamani ni ndoto
Wewe ni rubuni kwa penzi la kidani kama mtoto

  (CHORUS)

Yalinitesa mazoea aya lakini nishazoea mwaya
Ila tambua mapenzi mabaya, kidonda chake hakinanga dawa
Eeh mazoea aah, lakini mi nishazoea mwaya
Ila tambua mapenzi mabaya, kidonda chake hakinanga dawa

  (CHORUS)

No comments:

Post a Comment