Friday, February 19, 2016

NAONA BADO lyrics by Sudi and Amileena

Aah naona bora afadhali nioe mke basi muwe  wawili
Nimepungua yangu imani, wananicheka ona majirani
Penzi nilo kumwangia, utamu wa ndoa unaniishia (aaaah aah)
Wazazi wanaulizia, mpaka lini watasubiria eeeeeh
Nayaheshimu yako maamuzi, mara mbili fikiria
Ujana moshi hauna ujuzi, sote njia tunapitia
Nayaheshimu yako maamuzi, ooooh
Ujana moshi hauna ujuzi mke wangu eeeeh.....

  (CHORUS 1)
Naona bado, naona bado, hujaridhia kuishi na mimi
Naona bado, naona bado, ndo maana hutaki kuzaa na mimi ×2

Aiyaiya aiyaiyaiya....
Aiyaiya.... ×2

Mbona ugofya hadharani na matisho za mke wa pili
Najawa mie na majonzi, kwa kujua tena hauniamini
Naomba uwe na subira, sioni jinsi staki kukuzalia
Wakati wetu utafika, tuwe na sisi familia
Nayaheshimu yangu maamuzi, naomba penzi wewe subiria
Hili jambo nzito la uzazi, bado mie nalifikiria
Heshimu yangu maamuzi hoooo!!
Hili jambo si la ujuzi, bado mie nafikiria

  (CHORUS 2)
Naomba bado, naomba bado, muda hujafika kuzaa nawe
Naomba bado, naomba bado, subiri kidogo bwana wee ×2

Aiyaiya aiyaiyaiyaa...
Eeeeh eeeeh
Eeeeeeh!!!

Nimejaribu kukwambia, hebu tuzae hata mtoto mmoja
Majibu nimesubiria, sikuelewi daili unasema ngoja
Unaogopa kupoteza ujana, unataka tuishi kama jana
Eti bado mapema, kifungu gani cha ndoa kimesema...... (kipo)

Nayaheshimu yangu maamuzi naomba penzi wewe subiria
Hili jambo nzito la uzazi, bado mie nalifikiria

Nayaheshimu yako maamuzi, ooooh
Ujana moshi hauna ujuzi, mke wangu eeeeh

  (CHORUS 1&2)

Sudi we wacha papara (aaah)
Muda wetu utafika......

No comments:

Post a Comment