Showing posts with label KWETU lyrics by Raymond. Show all posts
Showing posts with label KWETU lyrics by Raymond. Show all posts

Thursday, April 14, 2016

KWETU lyrics by Raymond

Sifa kwa Mola wangu maulana, kwa mengi aliyoyafanya
Hadi mimi na wewe kukutana, kisuraa
Sijapanga kudanganyana, nasema ukweli mama
Kisa nakupenda sana, kisuraa
Unasema wanipenda, ila maisha yangu maseke
Michicha, milenda ndio menu yangu na ya kuku mateke
Yanichenga kila siku kilio salini nicheke
Sina tender ugali Buguruni mboga temeke
Nafurahi umeniridhia niwe nawe kimwali
Maisha yangu mtihani, nizoeshe maswali
Ukifika nyumbani vumilia, maana hali sio shwari
Asubuhi mchana pakavu, jioni ndio kula futari

  (CHORUS)
Tena
Uku kwetu muda wote mateja wanatinga
Viwaro vyetu ukifua kumbuka kuvilinda
Mwali wee uku kwetu muda wote mateja matinga
Swali wee swala la nyumba na gari, me bado, me bado
Ndo mwanza nimepanga, me bado, me bado
Sina hata kiwanja, me bado, me bado
Kulipa kodi majanga, me bado, me bado oooh

Mtaani kwetu hekaheka, ukienda sokoni kariri vichochoro
Ghetto la mkeka tu hakuna kitanda, shuka wala godoro
Hekaheka hakuna kibatari ndani giza totoro
Mvua ikinyesha, nyumba inageuka ka port ya comoro
Ila nimeshakupa, nimeshakupa mtima mtima
Ukija kususaa utanizika mzima mzima
Nimeshakupa eeh, nimeshakupa mtima mtima
Ukija kususa utanizika mzima mzima

  (CHORUS)