Thursday, July 21, 2016

YATAKWISHA lyrics by Ben Pol ft Linah

[Intro – Ben Pol]
(Burn Record!)
Na yatakwisha
Mmh aah ee

[Verse 1 – Ben Pol]
Ala moja haikai panga mbili nimeamini
Nilidhani nitaweza kuwamudu wote wawili
Ye awepo, na we niwe wako
Kwake nipate, na we nipate penzi lako
Kweli sitoweza, nikuache uende nibaki nilie
Bora kupoteza, mali nipate moyo wako nitulie
Kweli sitoweza, kuacha uende nibaki nilie
Bora kupoteza, vyote nipate moyo wako nitulie

[Chorus – Ben Pol] x2
Ulisema umeamua kunisamehe na yatakwisha
Leo tena unataka kunitesa na kuniumiza
Jua kwamba leo mi mwenzio, kesho wewe
Haya mateso unayonipa mi mwenzio, utapata kwa mwingine

[Verse 2]
[Linah]
Ukweli wote ulijificha hukuweka wazi
Fadhili zote kumbe bure nani atanienzi
Ningejua pendo lako wala nisingelipokea
Naumia, penzi hili sitaweza ku-share

[Ben Pol]
We ndo wa moyoni, siwezi ntafanya nini?
Kuishi mbali nawe, kwangu nami ni kazi bure
Labda uhai niutoe (niwe chizi nipagawe)
Kama timamu nielewe (naomba unisamehe)
Labda uhai niutoe (niwe chizi nipagawe)
Kama timamu nielewe (naomba unisamehe)

[Chorus – Ben Pol] x2
Ulisema umeamua kunisamehe na yatakwisha
Leo tena unataka kunitesa na kuniumiza
Jua kwamba leo mi mwenzio, kesho wewe
Haya mateso unayonipa mi mwenzio, utapata kwa mwingine

[Outro – Ben Pol]
Kwa mwingine, kwa mwingine
Uuh (mateso) ooh oo uuh
Clever, Sheddy Clever
Clever!
Mmh Ben Pol, Linah
Burn Records!

No comments:

Post a Comment